Kilimo cha Strawberry

Upatikanaji wa miche na matunda: 0752972727 au 0624001036
Utangulizi
Strawberry (fukasidi) hustawi katika maeneo yenye joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa zaidi, Hasa katika Green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 na zaidi kutoka usawa wa bahari. Zao hili hapa Tanzania hustawi zaidi katika mikoa mingi kama Morogoro, Mbeya, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, na Pia hufanya vizuri katika mikoa ya Pwani endapo utalima kisasa zaidi na kufuata maelekezo ya kitaalamu (Under controlled condition)
UDONGO
Strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi, Pia udongo unaotuamisha maji kama mfinyanzi sio mzuri sana kwa ustawishaji wa strawberry, Pima Udongo kabla ya kuanza kilimo sio kwa strawberry peke yake hata kwa mazao mengine
UPANDAJI
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house).
1. Katika upandaji wa strawberry kwenye green house Utahitajika kuwa na Mabomba yenye matundu(Plastic Pipe) Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
2. Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana
3. Tandika karatasi la nylon sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au sehemu ya kuhifadhia.
4.Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
5. Jaza kokoto, yenye mapande makubwa kiasi.
6 .Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea
UMWAGILIAJI
Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii ina maanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.
KUVUNA
Zao la strawberry huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki stroberi inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo ikshafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za kuvuna mfululizo.
Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwa
WADUDU na MAGONJWA
Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi. Kama vile;
WADUDU
Spider (two spotted) mite
~ Cluster caterpillar
~ Heliothis
~ Looper
~ Rutherglen bug
~ Cutworm
~ Aphids
~ Queensland fruit fly
MAGONJWA
🕷Lethal yellows
Mmea ulioathirika unaonyesha dalili zifuatazo;
√ Majani yaliyokomaa yanakuwa na rangi ya dhambarau na yana jinyonganyonga kwa upande wa juu na kusababisha kuangua chini.
√ Majani chipukizi yanakuwa na rangi ya njano katika kingo za jani na kupelekea kudumaa kwa kikonyo cha jani. Huu ugonjwa unapunguza nafasi ya jani kushindwa kujitengenezea chakula chake na hivyo mmea kudumaa na kupelekea kufa kwa mmea.
🕷 Mnyauko fusari (fusarium wilt)
Ugonjwa huu huunezwa na mbegu zenye huu ugonjwa na husambazwa na vimelea vya fangasi ambavyo vipo kwenye udongo. Ugonjwa huu hujitokeza Zaidi kwenye kipindi cha kiangazi na hushambulia sehemu za mirija ya mmea inayopitisha chakula hivyo mmea hukosa chakula na maji na hatimaye unyauka na kufa. Na shina la mmea ukipasua ndani unakuta lina rangi ya kahawia.
Kudhibiti
1. Tumia mbegu safi na bora.
2. Tumia dawa ya kuua wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na yenye ubora.
3. Choma masalia ya mazao ili kudhibiti uenezaji wa ugonjwa
4. Chagua mbegu ambayo ina uwezo wa kuhimili magonjwa.
MATUMIZI YA STRAWBERRY
Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo.
Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na:
~ Kuliwa kama tunda.
~ Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula.
~ Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi.
~ Kutengeneza marashi n.k.
Wasiliana nasi:0752972727

Comments

  1. Halo,I'm Helena Julio from Ecuador,I want to talk good about Le_Meridian Funding Service on this topic.Le_Meridian Funding Service gives me financial support when all bank in my city turned down my request to grant me a loan of 500,000.00 USD, I tried all i could to get a loan from my banks here in Ecuador but they all turned me down because my credit was low but with god grace I came to know about Le_Meridian so I decided to give a try to apply for the loan. with God willing they grant me  loan of 500,000.00 USD the loan request that my banks here in Ecuador has turned me down for, it was really awesome doing business with them and my business is going well now. Here is Le_Meridian Funding Investment Email/WhatsApp Contact if you wish to apply loan from them.Email:lfdsloans@lemeridianfds.com / lfdsloans@outlook.comWhatsApp Contact:+1-989-394-3740.

    ReplyDelete
  2. casino no deposit bonus codes, free spins no deposit bonus
    free spins no 3 3 토토 deposit bonus codes, free spins no deposit bonus code, Free mw88 spins 포커 용어 no 슬롯 deposit bonus codes 2020, 유흥가 Updated 2021:

    ReplyDelete
  3. Harrah's Casino Hotel & Spa - Mapyro
    Directions to 나주 출장마사지 Harrah's Casino Hotel & Spa (Harrah's Cherokee) with 밀양 출장샵 Mapyro. Harrah's Cherokee Valley 전주 출장샵 River 이천 출장마사지 Casino Resort. 광명 출장샵

    ReplyDelete

Post a Comment